Tuesday, 10 March 2015

KUOMBA KWA IMAN

Kiufupi Iman ni ni kuwa na uhakika wa  matarajio  ulionayo, akili na ufahamu wako  vinapata    picha halisi ya yale uyatarajiayo

 Kwa kawaida tunajua kuwa mwanadamu lazima uishi ukiwa na matarajio fulan fulani kulingana na wakati na hali halisi ya mambo. Kwa habari ya imani UHAKIKA  ni lazima .

Mgonjwa anapokunywa dawa ni matarajio yake kupona na kwakuwa huwa na matarajio mema yanambidisha  anywe kwa bidii ili apone.Alokata tamaa  hata dozi hawezi kumaliza maana hana uhakika wa kupona.

  Basi iman ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana  ya  mambo yasiyoonekana Ebr 11;1..


Unapoenda mbele za Mungu omba huku ukitarajia kupata kile unachokihitaji { Amwendeaye Mungu lazima aamini Ebr  11;6 } Kwa kutokuamin, kutakufanya usiombe kwa bidii maana huna matarajio mema .

Kuomba kwa imani kutakufanya umtafute sana Mungu na  sio miujiza maana wenigne kwa kutafuta miujiza wameingia ktk mambo yanayowajutisha na kuwaondolea amani. Muujiza au jambo unalolitaka Mungu aweza tenda kwa namna isiyo fikirika maana yeye hakaririki, muujiza mmoja huutenda kwa namna mbalimali si lazima alivyopokea mwenzio ndivyo utapokea, Omba kwa imani.

Kwa imani utaaumba mambo mema kwaajili yako

Kwa imani utaponywa/  utaepushiwa uharibifu na kufanywa mrithi wa haki. 

Kwa imani utatimiziwa haja ya moyo wako . 

utapita na kuishi mahali  paliposhindikana .

Kwa imani utatambua  vikwazo vya mafanikio yako.                

Kwa imani utamshinda adui

Kwa imani utapata familia bora  nk

Sunday, 8 March 2015

KUMCHA MUNGU







Kumcha Mungu, twaweza kueleza  kwa namna mbalimbali kulingana na mtu anavyoelewa .Kumcha
MUNGU ni zaidi ya  kuonesha  unyenyekevu wa hali ya juu sana mbele za  MUNGU.

  EBR  12; 28-29  Basi kwakuwa tunapokea ufalme  usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza , pamoja na unyenyekevu na kicho. Maaana Mungu wetu ni moto ulao.

 Jambo hili  la  kumcha  Mungu   linaweza kudhihirika ktk ibada au hata maisha ya kila siku . Hata hivyo kwaajili hii   twaweza kutofautisha wacha Mungu na  wasio  wacha . Mcha Mungu ametambua uwepo wa Mungu na  nguvu zake   , hukumu ya Mungu na mambo mengine ambayo humfunua MUNGU  kwake . kila mtu liko jambao  au mambo yanayomfanya atambue  uwepo wa Mungu na hukumu yake na hilo laweza kuwa sababu ya kumcha Mungu.
Zaid sana tutambue kuna ufalme usiotetemeshwa na kuyumbishwa ,hudumu hata milele . Kama falme za dunia tunaziheshimu bas uflme huu ni zaidi maana Mungu mwenyewe ni mtawala.


UBARIKIWE.