Tuesday, 10 March 2015
Sunday, 8 March 2015
KUMCHA MUNGU
Kumcha Mungu, twaweza
kueleza kwa namna mbalimbali kulingana na mtu anavyoelewa .Kumcha
MUNGU ni zaidi ya
kuonesha unyenyekevu wa hali ya juu sana mbele za MUNGU.
EBR 12;
28-29 Basi kwakuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe
na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza , pamoja na
unyenyekevu na kicho. Maaana Mungu wetu ni moto ulao.
Jambo hili
la kumcha Mungu linaweza kudhihirika ktk ibada au hata
maisha ya kila siku . Hata hivyo kwaajili hii twaweza kutofautisha
wacha Mungu na wasio wacha . Mcha Mungu ametambua uwepo wa Mungu
na nguvu zake , hukumu ya Mungu na mambo mengine ambayo
humfunua MUNGU kwake . kila mtu liko jambao au mambo yanayomfanya
atambue uwepo wa Mungu na hukumu yake na hilo laweza kuwa sababu ya
kumcha Mungu.
Zaid sana tutambue kuna ufalme usiotetemeshwa na kuyumbishwa ,hudumu hata milele . Kama falme za dunia tunaziheshimu bas uflme huu ni zaidi maana Mungu mwenyewe ni mtawala.
UBARIKIWE.
Sunday, 18 January 2015
KUKUMBUKWA NA MFALME
Wafalme ama marais wa dunia hii wana mambo mengi na makubwa na aghalabu si rahisi kuwakumbuka watu wa chini.
Kwa wakristo mfalme wetu ni Mungu mkuu na Yesu Kristo ambay kamwe hasahau wanaomkimbilia.
2Samweli 9:1—13
1 Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya yonathani?
Kwa muhtasari hii habari ya Mefibosheti kukumbukwa na Mfalme Daudi, Mefibosheti ni wa familia ya adui yake mkubwa Daudi, mfalme Sauli. Kwenye mstari wa 8 unasema ‘akasujudu, akasema mimi mtumwa wako ni nini, hata ukamwangalia MBWA MFU kama mimi?
Mefibosheti amekata tamaa kiasi cha kujifananisha na MBWA MFU. Mpendwa mbwa afapo huwa hakumbukwi na yeyote, mzoga wa Mbwa hupitiwa mbali na zaidi labda lipite gari la taka liuchukue dampo... na hivyo ndivyo anajiona Mefibosheti mbele ya mfalme.
Mefibosheti amekata tamaa kwa sababu;
1. Ni mlemavu na kwa desturi ya wayahudi anaonekana ni laana na hivyo kutengwa.
2. Ni mjukuu wa Sauli mfalme aliyeasi na kizazi chake chote kupukutika.
3. Mfalme Daudi alikuwa adui wa Sauli
4. Mefibosheti ni maskini sana si tu ulemavu bali ufukara.
Mefibosheti anapokumbukwa na mfalme kila kitu kinabadilika;
1. Kaitwa mezani pa mfalme. Hebu tufananishe mezani pa mfalme na mezani pa rais ikulu.
2. Kapewa nafasi ya kula na kunywa mezani pa mfalme (raisi)
3. Akapewa milki yote ya Sauli... kumbuka sauli alikuwa mfalme na mwenye utajiri mkubwa.
4. Kapewa wafanyakazi 36 yaani 1+15+20 kwa Siba, wanawe 15 na watumwa 20 wa siba
5. Akapewa haki ya kufanyika mwanamfalme (prince) wa Daudi.
Kristo anapokukumbuka anakukaribisha ule mezani pake, anakupa milki (mali), wafanyakazi na haki ya kufanyika mwanamfalme(Prince).
Mpendwa yapaswa sana kung’ang’ania sana kwa Mungu ili tukumbukwa kwani Mugnu hatazami tukoje na tunamiliki nini bali anaangalia tunavyoweza kushukwa kwake namna tunavyojiona si kitu bali yeye ndiye mwenye thamani na kila kitu kwetu
Nakutakia maisha ya imani na ushindi...
Bidii siri ya mafanikio
Mhu 9;10a
"Lolote mkono wako utakalopata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako;"
Watu wengi hawapendI umasikin na wakati mwingine kuwa na maombi ya kuutokomeza lakini pasipo kufanya kazi ni sawa na mtu asiye na maono.Bidii siri ya mafanikio
"Lolote mkono wako utakalopata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako;"
Watu wengi hawapendI umasikin na wakati mwingine kuwa na maombi ya kuutokomeza lakini pasipo kufanya kazi ni sawa na mtu asiye na maono.Bidii siri ya mafanikio
Thursday, 15 January 2015
Karibu
Bwana Yesu asifiwe
Mpendwa ninayo furaha kukukaribisha kwenye blogu yetu mpya ya Betheli Halisi. Lengo la blogu hii ni kuchapisha neno na masomo ya kiroho kwa ujumla, maneno yatakayomfanya mkristo aishi maisha ya imani na ushindi.
Chanzo cha jina la blogu hii ni kutoka Mwanzo 28:17-19
17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.
18 Yakobo akaondoka asubuhi na mapema,
akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha
kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.
19 Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.
Karibu sana
Neema ya Bwana Yesu Kristo iwafunike
wenu
Mwl. Mary
Subscribe to:
Comments (Atom)