KUOMBA KWA IMAN
Kiufupi Iman ni ni kuwa na uhakika wa matarajio ulionayo, akili na ufahamu wako vinapata picha halisi ya yale uyatarajiayo
Kwa kawaida tunajua kuwa mwanadamu lazima uishi ukiwa na matarajio fulan fulani kulingana na wakati na hali halisi ya mambo. Kwa habari ya imani UHAKIKA ni lazima .
Mgonjwa anapokunywa dawa ni matarajio yake kupona na kwakuwa huwa na matarajio mema yanambidisha anywe kwa bidii ili apone.Alokata tamaa hata dozi hawezi kumaliza maana hana uhakika wa kupona.
Basi iman ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana Ebr 11;1..
Unapoenda mbele za Mungu omba huku ukitarajia kupata kile unachokihitaji { Amwendeaye Mungu lazima aamini Ebr 11;6 } Kwa kutokuamin, kutakufanya usiombe kwa bidii maana huna matarajio mema .
Kuomba kwa imani kutakufanya umtafute sana Mungu na sio miujiza maana wenigne kwa kutafuta miujiza wameingia ktk mambo yanayowajutisha na kuwaondolea amani. Muujiza au jambo unalolitaka Mungu aweza tenda kwa namna isiyo fikirika maana yeye hakaririki, muujiza mmoja huutenda kwa namna mbalimali si lazima alivyopokea mwenzio ndivyo utapokea, Omba kwa imani.
Kwa imani utaaumba mambo mema kwaajili yako
Kwa imani utaponywa/ utaepushiwa uharibifu na kufanywa mrithi wa haki.
Kwa imani utatimiziwa haja ya moyo wako .
utapita na kuishi mahali paliposhindikana .
Kwa imani utatambua vikwazo vya mafanikio yako.
Kwa imani utamshinda adui
Kwa imani utapata familia bora nk
No comments:
Post a Comment