Kumcha Mungu, twaweza
kueleza kwa namna mbalimbali kulingana na mtu anavyoelewa .Kumcha
MUNGU ni zaidi ya
kuonesha unyenyekevu wa hali ya juu sana mbele za MUNGU.
EBR 12;
28-29 Basi kwakuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe
na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza , pamoja na
unyenyekevu na kicho. Maaana Mungu wetu ni moto ulao.
Jambo hili
la kumcha Mungu linaweza kudhihirika ktk ibada au hata
maisha ya kila siku . Hata hivyo kwaajili hii twaweza kutofautisha
wacha Mungu na wasio wacha . Mcha Mungu ametambua uwepo wa Mungu
na nguvu zake , hukumu ya Mungu na mambo mengine ambayo
humfunua MUNGU kwake . kila mtu liko jambao au mambo yanayomfanya
atambue uwepo wa Mungu na hukumu yake na hilo laweza kuwa sababu ya
kumcha Mungu.
Zaid sana tutambue kuna ufalme usiotetemeshwa na kuyumbishwa ,hudumu hata milele . Kama falme za dunia tunaziheshimu bas uflme huu ni zaidi maana Mungu mwenyewe ni mtawala.
UBARIKIWE.
No comments:
Post a Comment