Monday, 27 June 2016

NYAKATI /VIPINDI

Katika ulimwengu tulioao tunapita katika vipindi tofauti, na vipindi hivyo vina makusudi kwa Mungu.Kuna wakati wa kufurahi na wakati wa kulia, kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna. Watu wengi tunatazamia na tunapenda kufurahi kila wakati tule tunywe na kupata kila jema kutoka kwa Mungu lakini tunajikuta tunakumbana na nyakati tofauti hii ni kwasababu MUNGU ameweka kila wakati kwa makusudi yake.

Makusudi ya vipindi tofauti tunavyopitia wakati mwingine imekuwa fumbo kwa muhusika isipokuwa Mungu hutambua hilo maana ameamuru, na sihivyo tu wakati mwingine tunatambua kusudi la Mungu baada ya kuona matokeo.

Jambo la msingi  hapo ni kwamba tunatakiwa kujua kuwa katika kila wakati ambao Mungu anatupitisha tukazane kulijua na kulifuatilia kusudi la MUNGU ni nini haswa.Itatusaidia kujiepusha kwa mabaya yatakayotutoa uweponi mwa MUNGU....MUHUBIRI 3;1-7

MPANGO WA MUNGU

Mungu kama aisivyo ni Mungu wa mipango,tangu mwanzo Mungu amekuwa akienda kwa mipango. ukisoma kitabu cha mwanzo 1; Mungu alikuwa na mpango wa kuijaza dunia maana ilikuwa utupu na kuiptia Adamu na Hawa dunia ikipata vizazi  tofautitofauti.

Napenda tujikumbushe mpango wa Mungu ktk agano jipya Mungu anakusudia kuleta wokovu kwa mwanadamu baaada ya uasi, jambo ambalo Mungu alilifanya kurudisha mahusiano yake na mwanadamu ni kumtoa mwanae wa pekee Yohana 3;16-19. Wokovu ni mpango kamili wa Mungu kumkomboa mwanadamu, hakuna mwanadamu anaeweza kupata msamaha wa dhambi isipokuwa kwa  njia ya kuukubali wokovu.

Jinsi ya kuupata wokovu, ni kwanjia ya kumkiri yesu kwa kinywa chako Warumi 9;10 , na ukiri wako unadhihirisha kile ulichokiamini moyoni mwako. Kumwamini yesu yakuwa ni Bwana na mwokozi katika maisha yako maana kwa yeye wokovu unapatikana.

Ikiwa wokovu ndo mpango sahihi wa kumuokoa mwanadamu, hatutapona jehanamu bila huo japokuwa jambo la jehanamu limeonekana kuwa jambo la kufikirika lakini hukumu ipo kama vile tunavoamini kifo kipo tujitayarishe kukabiliana nayo...

NAWAPENDAAA