Mungu kama aisivyo ni Mungu wa mipango,tangu mwanzo Mungu amekuwa akienda kwa mipango. ukisoma kitabu cha mwanzo 1; Mungu alikuwa na mpango wa kuijaza dunia maana ilikuwa utupu na kuiptia Adamu na Hawa dunia ikipata vizazi tofautitofauti.
Napenda tujikumbushe mpango wa Mungu ktk agano jipya Mungu anakusudia kuleta wokovu kwa mwanadamu baaada ya uasi, jambo ambalo Mungu alilifanya kurudisha mahusiano yake na mwanadamu ni kumtoa mwanae wa pekee Yohana 3;16-19. Wokovu ni mpango kamili wa Mungu kumkomboa mwanadamu, hakuna mwanadamu anaeweza kupata msamaha wa dhambi isipokuwa kwa njia ya kuukubali wokovu.
Jinsi ya kuupata wokovu, ni kwanjia ya kumkiri yesu kwa kinywa chako Warumi 9;10 , na ukiri wako unadhihirisha kile ulichokiamini moyoni mwako. Kumwamini yesu yakuwa ni Bwana na mwokozi katika maisha yako maana kwa yeye wokovu unapatikana.
Ikiwa wokovu ndo mpango sahihi wa kumuokoa mwanadamu, hatutapona jehanamu bila huo japokuwa jambo la jehanamu limeonekana kuwa jambo la kufikirika lakini hukumu ipo kama vile tunavoamini kifo kipo tujitayarishe kukabiliana nayo...
NAWAPENDAAA
No comments:
Post a Comment