Sunday, 18 January 2015

KUKUMBUKWA NA MFALME


Wafalme ama marais wa dunia hii wana mambo mengi na makubwa na aghalabu si rahisi kuwakumbuka watu wa chini.
Kwa wakristo mfalme wetu ni Mungu mkuu na Yesu Kristo ambay kamwe hasahau wanaomkimbilia.
2Samweli 9:1—13
1 Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya yonathani?
Kwa muhtasari hii habari ya Mefibosheti kukumbukwa na Mfalme Daudi, Mefibosheti ni wa familia ya adui yake mkubwa Daudi, mfalme Sauli. Kwenye mstari wa 8 unasema ‘akasujudu, akasema mimi mtumwa wako ni nini, hata ukamwangalia MBWA MFU kama mimi?
Mefibosheti amekata tamaa kiasi cha kujifananisha na MBWA MFU. Mpendwa mbwa afapo huwa hakumbukwi na yeyote, mzoga wa Mbwa hupitiwa mbali na zaidi labda lipite gari la taka liuchukue dampo... na hivyo ndivyo anajiona Mefibosheti mbele ya mfalme.
Mefibosheti amekata tamaa kwa sababu;
1. Ni mlemavu na kwa desturi ya wayahudi anaonekana ni laana na hivyo kutengwa.
2. Ni mjukuu wa Sauli mfalme aliyeasi na kizazi chake chote kupukutika.
3. Mfalme Daudi alikuwa adui wa Sauli
4. Mefibosheti ni maskini sana si tu ulemavu bali ufukara.
Mefibosheti anapokumbukwa na mfalme kila kitu kinabadilika;
1. Kaitwa mezani pa mfalme. Hebu tufananishe mezani pa mfalme na mezani pa rais ikulu.
2. Kapewa nafasi ya kula na kunywa mezani pa mfalme (raisi)
3. Akapewa milki yote ya Sauli... kumbuka sauli alikuwa mfalme na mwenye utajiri mkubwa.
4. Kapewa wafanyakazi 36 yaani 1+15+20 kwa Siba, wanawe 15 na watumwa 20 wa siba
5. Akapewa haki ya kufanyika mwanamfalme (prince) wa Daudi.
Kristo anapokukumbuka anakukaribisha ule mezani pake, anakupa milki (mali), wafanyakazi na haki ya kufanyika mwanamfalme(Prince).

Mpendwa yapaswa sana kung’ang’ania sana kwa Mungu ili tukumbukwa kwani Mugnu hatazami tukoje na tunamiliki nini bali anaangalia tunavyoweza kushukwa kwake namna tunavyojiona si kitu bali yeye ndiye mwenye thamani na kila kitu kwetu

Nakutakia maisha ya imani na ushindi...

No comments:

Post a Comment